This is default featured slide 1 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 2 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 3 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 4 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

This is default featured slide 5 title

Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.

Thursday, October 18, 2012

Wazazi walia utitiri wa michango Marian Boys

WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya Marian Boys iliyoko Kerege, wilayani Bagamoyo, Pwani, wamelalamikia wingi wa michango katika shule hiyo ikiwemo ya ujenzi wa madarasa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii, baadhi ya wazazi wamesema uongozi wa shule hiyo unawatwisha hata majukumu ya mmiliki wa shule.
Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina wakihofia usalama wa watoto wao, wazazi hao walisema uvumilivu wao umefika kikomo.
Walisema hawana shida na karo na michango mingine kama chakula, sare na usafiri, bali kilio chao ni kitendo cha uongozi wa shule hiyo chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi ya shule hiyo aliyetajwa kwa jina moja la Heri kuwabebesha jukumu la mmiliki wa shule hiyo.
Walisema kila mtoto aliyekuwa akitaka kujiunga na kidato cha kwanza, alilipa sh 15,000 na wanafunzi 240 waliofaulu, walitakiwa kutoa sh 400,000 kabla ya kujiunga rasmi kwa masomo.
Walisema chini ya mpango huo, shule hiyo iliweza kutengeneza sh milioni 96 kwa ajili ya majengo, hivyo kubeba jukumu la mmiliki wa shule.
Kwa mujibu wa maelezo ya wazazi hao, uongozi wa shule uliwaeleza ni sehemu ya ada ambayo watalipa baada ya kujiunga na masomo rasmi shuleni hapo.
Wamedai kuwa baada ya watoto kuanza masomo, uongozi wa shule uliwataka kulipa ada kamili na kwamba sh 400,000 ni ada ya majengo.
Walisema jambo hilo liliwaweka kwenye wakati mgumu wazazi, lakini kwa kupenda elimu ya watoto wao, walikubali kulipa ada kamili kama ilivyotakiwa.
“Hapa tulianza kuwa na mashaka, lakini kwa kupenda elimu ya watoto wetu, tukaona basi, tuendelee, lakini hapana sasa imebidi tuseme,” alisema mmoja wa wazazi hao.
Alisema katika mazingira hayo, bado uongozi wa shule hiyo hivi karibuni uliitisha harambee ya kuchangia mabweni ya madarasa ya kidato cha tano na sita.
“Katika harambee ile, wazazi tulikuwa ni kama wahusika wakuu, kila mmoja alitakiwa kuahidi fedha, kwa mfano mimi niliahidi sh 100,000, lakini baada ya kutafakari sana, kwa kweli hadi sasa sijatoa,” alisema mzazi mwingine.
Alisema kilichowakera zaidi wazazi hadi kulalamika, ni hatua ya hivi karibuni ya uongozi wa shule hiyo kuwataka kila mzazi kuchanga sh 200,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa.
Wazazi hao walisema mapema wiki hii baadhi ya wazazi wametumiwa ujumbe mfupi wa simu ukiwalisha uamuzi wa mkutano wa wazazi uliofanyika Oktoba 6, mwaka huu, kwenye ukumbi wa Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam.
Kupitia ujumbe huo uliotumwa kwa simu namba 0713 431264, unaeleza kilichofikiwa kwenye kikao hicho kuwa kila mzazi anatakiwa kutoa sh 200,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na kwamba hadi ifikapo Desemba 31 mwaka huu wanatakiwa wawe wamekamilisha mchango huo kupitia akaunti ya shule na kwa maelezo zaidi wapige namba 0777523518.
Wazazi wamehoji mantiki ya uongozi na mmiliki wa shule hiyo waliyemtaja kwa jina moja la Father Bayo kuwachangisha wazazi hadi ujenzi wa madarasa ya shule hiyo binafsi.
Tanzania Daima ilipomtafuta mwenye namba hiyo 0777523518, alikiri yeye ni Heri, Mwenyekiti wa Kamati ya Wazazi wa shule ya Marian Boys.
Hata hivyo, wakati mwandishi wa habari hizo akieleza sababu ya kutafutwa kwake, simu ilikatika na kila alipotafutwa, ujumbe uliashiria alikuwa nje ya nchi.
Tanzania Daima ilipomtafuta mtumaji wa ‘meseji’ kwa wazazi, mhusika alijitambulisha kuwa ni mwalimu wa shule hiyo na alipotakiwa kutoa ufafanuzi, alisita kabla ya kumpasia simu yake aliyemtambulisha kama mkuu wa shule.
Naye mkuu wa shule, akakiri kwa ufupi uwepo wa mchango huo na kila mzazi anapaswa kulipa kupitia akaunti ya shule.
Alipoulizwa ni malipo gani hayo, alisita kidogo na kisha kusisitiza maelezo yalishatolewa.

CHANZO:TANZANIA DAIMA

Wednesday, October 17, 2012

Dk. Mwakyembe awataka Watanzania kuchangia elimu

WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kuchangia elimu, kama wanavyofanya katika harusi. Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati wa Mahafali ya Darasa la Saba na Shule ya Awali ya Shule ya Mwalimu Nyerere.

Alisema imekuwa jambo la kawaida kwa sasa, kukuta kundi la watu wamekaa kujadili michango ya harusi na kuacha elimu.

“Jamani mimi nimetembea sijaona mambo yanavyofanyika hapa Tanzania, majirani zetu tu hapo Kenya wanatushinda, Kenya hukuti watu wanachangisha harusi, kule ukikuta watu wamekaa ujue wanajadili suala la elimu.

“Hapa kwetu masuala haya ya harusi yanazidi kushamiri, zamani tulikuwa tunaona wasichana ndiyo wanafanyiwa kitchen party, lakini eti sasa hivi wanaume nao wanafanyia sijui begi party. Itafika mahali watu wataanzisha kaptula party.

“Watanzania tumeacha kabisa kuchangia elimu, tunaona harambee muhimu ni harusi, hebu tubadilike ndugu zangu, ukiona jirani yako au ndugu yako anashindwa kusomesha mtoto msaidie,” alisema Dk. Mwakyembe.

Aidha, alitoa wito kwa wanafunzi wa kike, kutokimbilia ndoa za utotoni na badala yake waweke juhudi katika masomo.

“Nawaasa wanangu wote, lakini zaidi ninyi wa kike ogopeni ndoa za utotoni, wekeni juhudi katika masomo mpate shahada nyingi zaidi, kwa kuwa sasa hivi tuko katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na ushindani wa ajira utakuwa mkubwa,” alisema Dk. Mwakyembe.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Shule ya Mwalimu Nyerere, Jenerali Ulimwengu, alisema shule hiyo imeweza kukua kwa haraka toka wanafunzi 32 ilipoanzishwa hadi sasa ina zaidi ya wanafunzi 1,000, ambapo wanafunzi 127 wamehitimu darasa la saba kwa mwaka huu.

Tuesday, October 16, 2012

Mkuu wa Mkoa ahimiza masomo ya sayansi



MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick, amewataka vijana waanze kusoma masomo ya sayansi, ili madaktari wengi waweze kupatikana. Sadick alitoa wito huo jana jijini Dar es Salaam, katika hafla ya Siku ya Afya ya Macho, iliyokuwa imeandaliwa na Benki ya Standard Chartered kwa kupitia mradi wake wa ‘kuona ni kuamini’.

Alisema kuwa, tatizo la upofu kwa binadamu linaweza kuepukika katika jamii yoyote ile bila hata kutumia gharama kwa kuzingatia usafi wa mazingira, lishe bora na kula matunda.

“Mkizingatia ushauri wa daktari na kufuata kanuni zote za afya, nadhani hakuna mtu atakayepata tatizo la macho hapa nchini, kwani haihitaji gharama yoyote.

“Kuna umuhimu mkubwa wa kuwapatia elimu ya upofu wananchi wote, ili walielewe kwani wakielewa hili, tatizo litapungua na kuisha kabisa japokuwa kuna wataalam wachache.

“Katika takwimu zizilizopo, zinaonyesha kuwa, kila mwaka zaidi ya Watanzania 75,000 wanapata upofu kutokana na sababu mbalimbali, hivyo Serikali ni jukumu lake kuongeza bajeti, ili kukabiliana na changamoto hiyo,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Tanzania Limited, Sabi Theobald, alisema kuwa, mbali na kuendesha shughuli za biashara, pia wamekuwa mstari wa mbele katika shughuli za kuleta maendeleo katika jamii.

“Zaidi ya watu 177,000 wameweza kunufaika na mradi huo ambao hadi sasa tumetumia Dola za Marekani milioni 87.

“Sisi tumekuwa tukiangalia maeneo makuu manne kama vile elimu, afya, vijana na mazingira na pia tumekuwa na miradi mikubwa ya kukabiliana na janga la Ukimwi chini ya mradi wa Living With HIV, Ugonjwa wa Malaria chini ya Nets for life na mengineyo,” alisema Theobald.

Pia alisema kuwa, ili kuendeleza mafanikio ya benki hiyo, wamejipanga kukusanya Dola za Marekani milioni 100 ifikapo mwaka 2020, kwa ajili ya mradi wa kuona ni kuamini.

CHANZO:GAZETI MTANZANIA

Friday, October 12, 2012

Serikali Yatangaza Ajira 9,226 Kwa Walimu wa Sekondari na Vyuo Nchini

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kati) akitangaza ajira kwa waalimu
--
Katika mwaka wa masomo 2009/10 jumla ya wanafunzi 19,652 walihitimu mafunzo ya ualimu wakiwemo ngazi ya shahada 12,120 na stashahada 7,532. Kati ya wanafunzi hao jumla ya wanafunzi 17,684 walihitimu na kufaulu masomo yao, wenye shahada wakiwa 12,095 na wenye stashahada 5,589.

Uchambuzi wa sifa za wahitimu 17,684 waliohitimu na kufaulu mitihani yao umeonesha kuwa jumla ya wahitimu 8,857 wametoka kazini (in-service). Idadi hiyo inajumuisha wenye shahada 7,437 (25 kutoka Zanzibar) na wenye stashahada 1,420. Walimu hao wamerudi kwa waajiri wao ili wapangiwe kazi kulingana na elimu yao. Aidha, kuna wahitimu 328 kutoka Zanzibar (wakiwemo 303 tarajali na 25 kutoka kazini) ambao wanatarajiwa kuajiriwa katika shule na vyuo vya Zanzibar. Hivyo, wahitimu wanaobakia ambao wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu Tanzania Bara ni 8,524 wakiwemo wenye shahada 4,355 na wenye stashahada 4,169.
Kama ilivyobainishwa katika sehemu ya kwanza ya taarifa hii, jumla ya wahitimu 8,524 waliohitimu na kufaulu mitihani yao wataajiriwa na Serikali katika mwaka huu wa fedha. Vilevile Serikali imekubali kuajiri walimu 702 (wakiwemo 565 wenye shahada na 137 wenye stashahada) waliomaliza mafunzo yao miaka ya nyuma ambao wameomba kuajiriwa Serikalini.
Hivyo, jumla ya walimu wote watakaoajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2010/2011 ni 9,226 wakiwemo wenye shahada 4,920 na wenye stashahada ni 4,306. Kati ya walimu watakaoajiriwa jumla ya walimu 9,039 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari na walimu 187 wamepangwa kufundisha katika vyuo vya ualimu.

Walimu wote wa shule za sekondari wamepangwa katika Halmashauri mbalimbali kwa kutumia kigezo cha upungufu wa walimu katika Halmashauri husika. Hivyo, kila mwalimu anatakiwa kuripoti katika Halmashauri aliyopangwa kwa kuwa fedha za mshahara wake zimekasimiwa kwenye Halmashauri alikopangwa na si vinginevyo. Orodha ya walimu hao na Halmashauri walikopangwa zimetumwa kwenye Mikoa na Halmashauri. Aidha, orodha hiyo inapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi www.moe.go.tz na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa www.pmoralg.go.tz.

Walimu wote wapya wanaagizwa kuhakikisha kwamba wanaripoti katika Halmashauri/ Vyuo vya Ualimu walikopangwa ifikapo tarehe 24/01/2011. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.
Mwalimu yeyote atakayeshindwa kuripoti kwenye Halmashauri / Chuo alikopangwa baada ya siku saba (7) tangu tarehe anayotakiwa kuripoti atahesabika kuwa amekataa kukubali nafasi ya ajira aliyopewa na Serikali.

Baada ya kuripoti kwenye Halmashauri/Vyuo waajiri watatakiwa kuwajazia walimu hao Fomu maalum zenye Taarifa ya Kiutumishi ya Mtumishi (Personal Data Form)na kuziwasilisha Ofisi ya Rais, UTUMISHI pamoja na barua ya ajira ya mtumishi. Taarifa hizo zikiwa katika “hard” na “soft copy” ziwasilishwe UTUMISHI kabla au ifikapo tarehe 29/01/2011 ili watumishi hao waingizwe katika mfumo wa malipo (Payroll). Waajiri wanakumbushwa kwamba “Computer Data Sheet” hazitahitajika katika zoezi hili.

Waajiri(Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu–Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi)watawalipa malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia utumishi mwema katika Sekta ya Elimu.

Imetolewa na:

MHE. DKT.SHUKURU J. KAWAMBWA
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
 

Maofisa Elimu washitakiwa kwa wizi wa mishahara

Kaimu Maofisa Elimu wanne wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Juhudi na Ukonga, jijini Dar es Salaam, wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kushindwa kufanya uhakiki wa mishahara ya walimu 23, kutumia madaraka vibaya na kuiba Sh. milioni 11.8 zikiwa ni mali ya serikali.

Washtakiwa hao walifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Agnes Mchome, Jana.

Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Allen Kasamala, aliwataja Makaimu Maofisa Elimu hao kuwa ni Elizabeth Thomas, Mercy Nyalusi na Joseph Kaika.

alimtaja Mwalimu Mkuu wa Shule hizo kuwa ni Simon Jerome na Clara Nyongeja aliyeajiriwa na Wizara ya Fedha kama mtaalamu wa kompyuta.

Inadaiwa kuwa mshitakiwa Elizabeth na Mercy hawakuweza kupanda kizimbani baada ya kuuguwa ghafla kazini kabla ya kufikishwa mahakamani.

Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mchome jana, Kasamala alidai kuwa Februari 2010, washitakiwa walitumia madaraka yao vibaya kwa kushindwa kufanya uhakiki wa masalia ya mishahara ya walimu 23 yenye thamani ya Sh. 11,825,000.

Kasamala alidai mashtaka sita yaliyobaki yote yanamkabili Mwalimu Jarome.

Alidai kwa kutumia madaraka yake vibaya, Machi Mosi, mwaka juzi alimlazimisha Mwalimu George Masinde wa Shule ya Msingi Ukonga ampe Sh. 3,900,000 katika masalia ya mishahara yake.

Kasamala alidai pia kuwa Machi 2, mwaka juzi, Jarome alimlazimisha Bahati Saidi, ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Ukonga ampe Sh. 3,895,000 kutoka katika masalia ya mishahara yake.

Alidai katika tarehe hiyo hiyo, Mwalimu Jerome alimlazimisha Mwalimu mwingine wa Shule hiyo, Ester Mdachi, ampe Sh. 4,030,000 kutoka katika masalia ya mishahara yake ili kujinufaisha.

Mwendesha mashtaka huyo alidai Machi 3, mwaka juzi, mshtakiwa huyo kwa kutumia madaraka yake vibaya alimlazimisha Mwalimu Mwaija Chowo wa Shule ya Msingi Ukonga atoe katika masalia ya mishahara yake Sh. milioni 3 ampe.

Alidai pia kuwa Jarome aliiiba Sh. 11,825,000 Machi 3, mwaka juzi, zikiwa ni mali ya serikali na kwa njia ya rushwa mshtakiwa huyo alijipatia Sh 3,000,000 kutoka kwa Mwaija Chowo ikiwa ni kishawishi cha kutomchukulia hatua kwa kukataa kumkabidhi masalia ya mishahara yake.

Washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo, upelelezi haujakamilika na Hakimu Mchome alikubali wadhaminiwe kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mfanyakazi katika ofisi inayotambulika na wasaini dhamana ya Sh. milioni 5.

Kasamala aliomba mahakama itoe hati ya kuwaita washitakiwa wasiofika mahakamani wafike ili wasomewe mashitaka yanayowakabili.

Hakimu alikubali kutoa hati hiyo, washitakiwa waliofikishwa mahakamani walidhaminiwa na kesi iliahirishwa hadi Oktoba 24 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

CHANZO: NIPASHE